Jumatatu , 5th Dec , 2022

Mwili wa mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Muksini, ambaye ni mfanyabiashara wa bucha umekutwa kwenye gari yake katika eneo la Uwanja wa Fisi Maduka 9 jijini Mwanza, akiwa amefariki huku ikisadikika kunyongwa na kamba ambayo ilikutwa ndani ya gari hiyo

Gari ambalo limekutwa na mwili wa mfanyabishara Muksini

Wakizungumza katika tukio hilo, baadhi ya mashuhuda wamesema  majira ya saa 2:00 asubuhi wamelikuta gari hilo likiwa kandokando mwa barabara huku mwili huo ukiwa ndani ya gari.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa, amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akisema bado uchunguzi unaendelea kufanyika ili kubaini chanzo cha tukio hilo.