
Mhe.Jafo akiongea Bungeni mjini Dodoma
Mhe. Jafo ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu mswali ya mbunge wa Ilemela jijini Mwanza Mhe. Kiteto Koshumaswa alioyetaka kujua juhudi za serikali katika kukabiliana na uchache wa madawati unaopelekea wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la tatu kukaa chini katika shule za msingi nchini hasa kwa mikoa iliyo pembezoni mwa nchi.
Akijibu swali hilo, Mhe. Jafo amesema Serikali imefanya juhudi mbalimbali za kuhakikisha ukosefu wa madawati kwa wanafunzi wa shule za msingi unafika mwisho kwa kuwaagiza wakuu wa mikoa kufanikisha upatikanaji wa mawadati kabla ya mwaka ujao wa fedha katika halmashauri zote nchini.
Mhe.Jafo amesema serikali inaendelea kushughulikia changamoto zilizopo katika shule za msingi nchini ya ameahidi kufanya ziara ya kushtukiza katika halmashauri ili kuangalia kama wakurugenzi wa Halmashauri nchi wanatekeleza maagizo ya wizara yake.