Jumanne , 13th Nov , 2018

Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Salma Kikwete ameibua hoja juu ya utaratibu wa kuimba wimbo wa taifa kwa kile alichokidai kuwa watanzania wengi hawana uelewa wa kutosha juu ya wimbo huo.

Mke wa Rais Mstaafu awamu ya nne, Salma Kikwete.

Salma Kikwete ameuliza swali hilo katika mkutano wa 13 kikao cha sita cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha tatu ambapo alihoji juu ya taratibu rasmi za kuimba wimbo wataifa, swali lililoelekezwa kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, .

"Nchi zote duniani zina wimbo wake wa taifa na zina taratibu rasmi za kuimba mheshimiwa spika utarattibu ni upi kuhusu kuimba wimbo wetu wa taifa?," amehoji mama Salma.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje na Afrika Mashariki,Damas Ndumbaro, amesema taratibu wakati wa kuimba wimbo wa taifa ni lazima kila mtu kufuata taratibu za kijeshi.

"Mheshimiwa Naibu Spika utaratibu wa kuimba wimbo wa taifa, tunafuata ukakamavu wa kijeshi, tunaweka mikono chini na tunafuata taratibu a kijeshi," amejibu Dkt.Ndumbaro.

Mama Salma Kikwete ni mke wa Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete ambaye aliteuliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwa mbunge mwezi Machi mwaka jana , akiungana na mwanaye, Ridhiwani Kikwete ambaye ni mbuge wa Jimbo la Chalinze.