Jumanne , 5th Dec , 2023

Serikali imesema chanzo cha maporomoko ya matope wilayani Hanang mkoani Manyara ni kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ulikuwa na miamba dhoofu iliyonyonya maji na kusababisha mporomoko na hivyo kutengeneza tope.

Matope yaliyotapakaa kwenye makazi ya watu

Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kwamba sehemu iliyonya maji ilizua mgandamizo na sehemu ya mlima kushindwa kuhimili na kusababisha kumeguka kwa sehemu hiyo ambayo ilitengeneza tope lililoanza kuporomoko na kuanza kuzoa mawe na miti na kwenda kushambulia makazi ya wananchi katika maeneo hayo.

Aidha ameongeza kuwa serikali ilifuatilia taarifa za matetemeko kuanzia Septemba mwaka huu hadi siku ya tukio na kubaini kuwa hakukuwa na tetemeko lolote wala mlipuko wa volkano.