Jumatano , 25th Nov , 2020

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokarsia na Maendeleo, (CHADEMA), John Mnyika, amesema kuwa kitendo cha Halima Mdee, kusema kuwa kitendo cha wao kwenda kula kiapo cha ubunge wa viti maalum kimebarikiwa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe siyo cha kweli.

Kushoto ni Halima Mdee na kulia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 25, 2020, wakati akieleza hatua zilizochukuliwa na chama hicho, kufuatia maamuzi ya wanachama wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa BAWACHA Halima Mdee, kula kiapo Bungeni ili hali chama hicho hakikuridhia na wala hakikuwachagua.

"Kauli iliyotolewa jana wakati wa kuapishwa, iliyotaka kujenga ishara kama vile Mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe, alihalalisha hili linaloendelea, hiii kauli siyo ya kweli na yeye ndiye atakayeongoza kikao cha Kamati Kuu ya Chama kitakachofanyika Novemba 27, kwa kuwasikiliza wahusika kwanini waliamua kushiriki kwenye huu usaliti na nini kiliwasukuma kufanya hivyo", amesema Mnyika.

Jana mara baada ya kuapishwa Mdee alisema kuwa "Nikishukuru chama changu cha CHADEMA, kikiongozwa na Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe, ambao kupitia wao sisi tumepata nafasi ya kukiwakilisha chama chetu, viti hivi siyo hisani ila ni sehemu ya ushindi mkubwa ambao chama chetu kilipata".