Jumatano , 21st Feb , 2018

Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Nyasa, Mch. Peter Msigwa amewataka waombolezaji waliofika kwenye msiba wa Kiongozi wa chama hicho Kata ya Hananasif Kinondoni, Danie John kutokata tamaa na kuwaambia hakuna mtu atakayeishi milele duniani.

Mchungaji Msigwa amesema hayo leo ambapo amewaomba waombolezaji kutokata tamaa na kuendelea kupigania haki ya kidemokrasia ambayo John ameipigania hadi mwisho wa maisha yake.

Aidha Msigwa amesema kwamba kifo cha John kimetokana na shughuli zake za kisiasa lakini hali hiyo isiwakatishe tamaa katika kupambania demokrasia.

Kwa upande wa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu amepoteza maisha akipigania haki ya kidemokrasia. "Tunaamini John amefariki akitimiza majukumu yake ya kupiga kampeni kutafuta kura kwa ajili yangu na chama chake akipendacho,"

Aidha Mwalimu amesema kwamba endapo utamaduni wa miili ya watu kuokotwa ufukweni ukichwa utaandaa kizazi kitakacholipa kisasi. 

John alikuwa Katibu wa Chadema, Kata ya Hananasif, Kinondoni, Dar es salaam na mwili wake uliokotwa ufukweni mwa bahari ya hindi ambapo ulikuwa na majeraha ya kupihwa na kitu baada ya kutoweka Februari 11.