Jumapili , 21st Aug , 2022

Msemaji Mkuu wa serikali Gerson Msigwa, amesema kuwa kuna upotoshaji mkubwa kuhusu tozo za miamala ya kielektroniki iliyoanza katika mwaka huu wa fedha (2022/23) na kusema serikali imepunguza kwa kiasi kikubwa tozo hizo.

Msemaji Mkuu wa serikali, Gerson Msigwa

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Msigwa, amesisitiza kuwa Wizara ya Fedha itatoa ufafanuzi kuhusu tozo hizo na namna zilivyoleta nafuu kwa wananchi na kuwaomba watanzania kuwa watulivu.

"Kuna upotoshaji mkubwa kuhusu tozo za miamala ya kielektroniki iliyoanza katika mwaka huu wa fedha (2022/23), serikali imepunguza kwa kiasi kikubwa tozo hizo, Wizara ya Fedha itatoa ufafanuzi kuhusu tozo hizi na namna zilivyoleta nafuu kwa wananchi, naomba tutulie," amesema Msemaji Mkuu wa Serikali