
Mimba za utotoni
Akizungumza kwa masikitiko makubwa mtoto huyo amesema kuwa, wazazi wake wote wawili walifariki na kuchukuliwa na ndugu ambao walimwambia aende akaishi na kijana huyo, bila kujali ni mwanafunzi na pia umri wake ni mdogo.
Consolata Mlaponi ni mmoja kati ya watu waliojitolea kumsaidia mtoto huyo ambapo amesema kuwa kwa sasa mtoto huyo anakabiliwa na hali ngumu ya kimaisha, ikilinganishwa na umri wake ambao ni mdogo na hawezi kujitafutia.
Huku Jeshi la Polisi mkoani humo likianzisha oparesheni kabambe yenye lengo la kuwabaini na kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.