
Nyumba iliyoteketea kwa moto, mkoani Kagera.
Wakizungumza na EATV wananchi wa eneo la Bunena katika Manispaa ya Bukoba kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani humo, wameeleza kuwa walifanikiwa kuokoa maisha ya mtoto huyo aliyeachwa peke yake akiwa amelala.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, wamesema kuwa mtoto huyo aliachwa na mama yake akiwa amelala na kuwa wakati nyumba hiyo ya kupangisha iliyokuwa na familia sita, wakati inaanza kuteketea hata majirani wa mama huyo hawakuwepo.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kagera, Hamis Dawa, amesema kuwa mtoto huyo amepata majeraha ya moto na kukimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa, huku akiwatupia lawama wananchi kwa kuchelewa kutoa taarifa pindi ajali za moto zinapotokea.