Jumapili , 28th Aug , 2022

Jeshi la polisi mkoani Kigoma linamshikilia mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Taimu Kaogoma mkazi wa Kijiji cha Gwanupu wilayani Kakonko mkoani humo  kwa Tuhuma za kukutwa na viungo vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu ikiwemo fuvu la kichwa na mfupa wa taya.

Kamanda wa Polisi Kigoma ACP Felomon Makungu

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa Kamanda wa Polisi Kigoma ACP Felomon Makungu amesema mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 39 alikamatwa Agosti 25 mwaka huu wakati jeshi hilo likiwa katika ya kuzua uhalifu.

Aidha Kamanda Filemon amesema aina hiyo ya matukio imekuwa ikijirudia mkoani Kigoma kutokana na kuwepo kwa baadhi ya watu wanaoamini kufanikiwa kupitia imani za kishirikana na hivyo akawataka wakazi hao kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kudhibiti vitendo hivyo.