
Mbu aina ya Aedes Egypti anayesambaza virusi vinavyoambukiza homa hatari ya dengue.
Akiongea na East Africa Radio kiongozi wa Idara ya Magonjwa ya Nje Dkt. Mrisho Lupinda amethibitisha kutokea kwa kifo hicho cha mgonjwa wa dengue, katika hospitali hiyo ambayo imeshapokea jumla ya wagonjwa 154 tangu kuanza kwa ugonjwa huo..
Aidha, Dkt. Lupinda amewataka wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuchukua tahadhari na kuwaona wataalamu wa afya pindi wanapohisi wana dalili za ugonjwa huo.