Jumapili , 5th Jun , 2016

Mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, amesema kuwa bondia Muhammed Ali kwa hakika alikuwa bingwa ambaye atakumbukwa na wengi.

Trump ameyasema hayo Katika risala yake ya rambirambi kufuatia kifo cha bondia huyo maarufu duniani.

Kwa upande wake mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic, Seneta Bernie Sanders, amemshutumu Donald Trump na kumtaja kuwa mnafiki kutokana na kauli ambazo amewahi kuzitoa kuhusu waumini wa dini ya kiislamu.

Mwaka Jana, Marehemu Ali alilaani kauli iliyotolewa na Donald Trump, ya kuwazuia kabisa waislamu kuingia nchini Marekani.

Muhammed Ali alifariki Ijumaa huko Arizona, ambapo aliugua maradhi ya kusahau- sahau, kwa zaidi ya miaka thelathini.

Chanzo BBC