Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni akila kiapo leo , Mei 12, 2021
Rais Museveni anaiongoza nchi ya Uganda kwa muhula mwingine tena, na huu ukiwa ni muhula wake wa sita tangu alipoingia madarakani mwaka 1986, kwa mapinduzi ya kijeshi.
Akizungumza mara baada ya kuapishwa Rais Museveni amesema hawatoitilia maanani mihadhara inayohusu suala zima la demokrasia ya nchi hiyo kutoka katika nchi za kigeni bali ile inayotoka barani Afrika
Pia Rais Museveni amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuruhusu Sukari kutoka nchini humo kuingia Tanzania huku akisema kuwa kwasasa Uzalishaji bidhaa nchini Uganda ni mkubwa.
Zaidi ya marais 10 kutoka Mataifa mbalimbali wameshiriki shughuli ya uapisho huo, akiwemo Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.