Jumanne , 23rd Feb , 2016

Utafiti unaeleza kuwa sababu inayofanya Thamani ya Shilingi nchini Tanzania kushuka ni pamoja na muundo wa uchumi wa nchi unaofanya mahitaji ya dola na fedha za kigeni unakuwa makubwa kuliko fedha za Tanzania kwa kuagiza zaidi bidhaa kutoka nje.

Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya kutafiti na kupunguza umaskini nchini Dkt. Donald Mmari

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya kutafiti na kupunguza umasikini nchini Dkt. Donald Mmari kwenye mazungumzo na East Africa Television na kuongeza kuwa ni lazima serikali iongeze uzalishaji wa ndani ili iweze kutumia bidhaa za ndani zaidi na kupunguza mahitaji ya kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi.

Dkt. Mmari ameongeza serikali ni Lazima irekebishe sera zake za muda mrefu za uchumi huku akibainisha kuwa thamani ya shilingi ya Tanzania katika miaka miwili iliyopita imeporoka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Aidha Dkt. Mmari amesema kuwa sababu nyingine ya kushuka kwa shilingi ni kutokana na kshuka kwa mahitaji ya soko la dunia ambapo nchi nyingi ambaz\o tunaziuzia bidhaa zetu zilikumbwa na mdororo wa kiuchumi.

Ametolea mfano wa soko la dhahabu nchini ambayo inazalishwa kwa wingi nchini imepungua kutoka shilingi 1,700 ya hapo awali mpaka shilingi 1,200 kitu ambacho kinafanya fedha za kigeni kuingia kwa uchache nchini.