Ijumaa , 6th Dec , 2019

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imetoa tahadhari ya mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha, katika Mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba huku Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe na Iringa mvua zikiendelea kunyesha.

Mvua ikinyesha

Tahadhari hiyo imetolewa kufuatia kuwepo kwa uwezekano wa kutokea Vimbunga pacha, muda wowote kuanzia leo Disemab 6, 2019, katika ukanda wa Bahari ya Hindi kutokana na kuwepo kwa migandamizo midogo ya hewa.

"Tahadhari ya vipindi vifupi vya mvua kubwa kwa maeneo machache ya Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na angalizo la mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba,Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe inaendelea" imeeleza taarifa hiyo.

Aidha mamlaka hiyo imewashauri wananchi, kufuatilia taarifa za utabiri kutoka katika Mamlaka hiyo na kuzingatia tahadhari zinazotolewa.