Alhamisi , 15th Sep , 2022

Mwili wa Maria Baso (24) mwanachuo aliyeuawa na kikundi cha wahalifu wanaodhaniwa kuwa 'Panya road' usiku wa kuamkia Septemba 14,2022, unatarajiwa kuzikwa jumamosi ya Septemba 17, 2022 Mwenge jijini Dar es Salaam, huku wazazi wakiendelea kuomba vyombo usalama kukomesha vitendo hivyo.

Maria Baso, aliyeuawa na panya road

Akizungumza na EATV mama wa Marehemu Maria, Bi. Cecilia Marko ameeleza kuwa taratibu za mazishi zimeanza kufanyika.

Kwa undani wa taarifa hii usikose kutazama EATV SAA 1 leo Septemba 15,2022.