Ijumaa , 3rd Jul , 2020

Mwanaume mmoja anayefahamika kama Felix Rwechungura mkazi wa Isamilo Msikitini, mkoani Mwanza, anatuhumiwa kuwabaka na kuwalawiti kwa nyakati tofauti, watoto watano wenye umri wa miaka sita na miaka saba na kuwaharibu vibaya.

Ukatili

Imeelezwa kuwa baba huyo mwenye umri wa miaka 50, anatuhumiwa kuwabaka watoto hao bila huruma, ambapo mke wake Janeth Steven amesema kuwa mume wake huyo kwa muda mrefu, watoto wengi wa hapo mtaani walikuwa wakimuogopa.

Aidha baaadhi ya watoto wanaodaiwa kufanyiwa kitendo hicho wamesema kuwa, mwanaume huyo alikuwa akiwaita na kuwapeleka chumbani kisha kuwalazimisha kuwavua nguo, na baada ya hapo huwafunga kamba na kisha kuwalazimishwa kuwaingilia kimwili.

Yassin Ally ni Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za watoto na wanawake, amewaomba wazazi kuzungumza na kuwakagua watoto wao ili kubaini changamoto zinazowakabili.