Jumamosi , 4th Sep , 2021

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Ruvuma Jackline Msongozi, amesema kipindi anaomba nafasi ya uongozi watu walimdharau na kumuambia yeye ni Mama Ntilie tu hajasoma hawezi kuwa kiongozi leo anafanya mambo makubwa ya kuusaidia mkoa wa Ruvuma pamoja na Taifa kwa ujumla.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Ruvuma, Jackline Msongozi

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wananchi pamoja na wakulima wa mkoa wa Ruvuma.

"Wakati naingia madarakani wapo walionidharau kwamba sijasoma, lakini wakati naomba hiyo nafasi niliguswa moja kwa moja na shida za wanawake na wananchi wengine wadogo wadogo katika masuala ya kilimo, ndiyo maana nilisema nijitahidi nifanye kazi ili wale waliokuwa wanadharau waone nimefanya hata robo," amesema Mbunge Jackline.