Jumatatu , 22nd Aug , 2022

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Mwigulu Nchemba, ameziomba taasisi za dini kuendelea kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan, ili aendelee kuiongoza nchi vizuri na kutimiza dira yake ya uwekezaji katika sekta ya uzalishaji, kutengeneza ajira, kukuza uchumi na kujenga Tanzania yenye umoja.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Mwigulu Nchemba

Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo mkoani Singida aliposhiriki katika Jubilee ya miaka 50 ya Jimbo Katoliki Singida na kusema Rais Samia ana dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo wananchi wake, hivyo ni vema kumuombea ili yale aliyodhamiria kwa ajili ya nchi yaweze kutimia.

Aidha amesema kuwa taasisi za dini zina mchango mkubwa katika kuchochea maendeleo ya jamii katika sekta mbalimbali za maendeleo zikiwemo za afya, maji na elimu hususani maeneo ya pembezoni.