Jumanne , 13th Jul , 2021

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, amewahakikishia Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Jumuiya ya Kimataifa kwamba serikali iko katika hatua za kupunguza viwango vya kodi zinazotozwa ili kusisimua zaidi uchumi na kuondoa malalamiko yaliyotolewa na jumuiya hiyo.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba

Dkt. Nchemba ametoa ahadi hiyo Jijini Dar es Salaam alipokutana na Jumuiya hiyo ya Kimataifa kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyojitokeza kwenye Bajeti Kuu ya Serikali iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.