Jumatatu , 12th Dec , 2016

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwiguli Nchemba amesema kuwa huenda watu waliokutwa wamekufa na kutupwa kwenye mto Ruvu kwa kufungwa kwenye viroba walikuwa ni wahamiaji haramu ambao walikumbwa na mkasa huo toka kwa wasafirishaji wa wahamiaji hao.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba.

 

Akizungumzia tukio hilo leo Mkoani Singida Waziri Mwigulu amesema kitendo cha kukutwa kwa wahamiaji zaidi ya 80 wakiwa na majeraha na hawajiwezi mkoani Pwani kinahusisha kwa namna au nyingine na maiti zilizookotwa mto Ruvu

Waziri Mwigulu amesema kuwa watu hao ambao wamezikwa na serikali licha ya ndugu au taifa lolote kujitokeza sheria inawaruhusu kufanya hivyo kutokana na kutokutambulika kwa watu hao.

Mhe. Mwigulu amesema bado wanaendelea na uchunguzi juu ya matukio hayo ikiwa na operesheni mbalimbali za kutokomeza matukio ya kihalifu pamoja na wahamiaji haramu nchini.