Jumatano , 7th Oct , 2015

Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), marehemu Christopher Mtikila unatarajiwa kuagwa leo katika ukumbi wa kareemjee Jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea mkaoni Njombe wilayani Ludewa.

aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Democrat Party (DP), Marehemu Christopher Mtikila

Mchungaji Mtikilia alifariki dunia Oktoba 4, mwaka huu kwa ajali ya gari katika kijiji cha Msolwa, Chalinze mkoani Pwani akitokea kwenye kampeni za uchaguzi za wagombea wa chama chake nafasi za udiwani na ubunge jimbo la Njombe Kusini.

Kwa mujibu wa msemaji wa familia Victor Manyai amesema kuwa ratiba ya kumuaga mchungaji mtikila itaanza saa tatu asubuhi na kuishia saa saba kwa kuagwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali na vyama.

Marehemu Mtikila atakumbukwa kwa historia yake ya kuwa na msimamo wa kuidai Tanganyika ikiwa ni pamoja na kudai katiba itambue uwepo wa mgombea huru.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa chama hicho amesema kuwa ili kumuenzi mchungaji mtikila wataendelea kusimamia kesi alizoziacha mahakama ikiwemo ile ya kupinga tume kumuengua katika kinyang'anyiro cha kugombea urais lakini na kesi ya kupinga mgombea urais wa CHADEMA, Edward Lowassa kwa madai alianza kampeni kabla ya wakati.