Jumatatu , 21st Nov , 2022

Mtu mmoja aliyekadiriwa kuwa na umri wa 30 mpaka 35 amekutwa amefariki  katika Bwawa Dogo lililopo katika Msitu wa TANWAT  Eneo la Kibena Mjini Njombe

Walinzi katika Msitu ya TANWAT uliopo karibu na Bwawa  hilo wamesema majira ya saa 11:10 Alfajiri ya Novemba 21 waligundua uwepo wa mtu ambaye alikuwa  akisogea katika bwawa  Hilo huku akiwa ameshika tochi na baada ya kufika akaanza kuingia ndani ya bwawa hilo na hata walipojaribu kumuita ili atoke nje ya bwawa hakuwasikiliza

Baada ya Mwili Huo Kutolewa katika Bwawa Jeshi  la Zimamoto limewataka wananchi kuutambua Mwili huo lakini Wananchi  wamekiri kutomfahamu mtu  huyo.