Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Naibu Waziri Mkuu aivunja bodi ya ETDCO

Ijumaa , 29th Mar , 2024

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameagiza kuvunjwa kwa Bodi ya Kampuni Tanzu ya TANESCO ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme (ETDCO) na kuundwa upya Menejimenti ya Kampuni hiyo kutokana na utendaji kazi mbovu.

Dkt. Doto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Mbali na utendaji mbovu, wizi  fedha za umma ndani ya Shirika pamoja na wizi  wa vifaa vya umeme uliokithiri umetajwa pia kama miongoni mwa sababu zilizopelekea bodi hiyo kuvunjwa. 

Dkt. Biteko ametoa agizo hilo wakati wa Kikao kazi baina yake na Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kampuni zake tanzu, Wakurugenzi wa TANESCO wa Kanda na Mameneja wa Mikoa ambacho kimefanyika tarehe 28 Machi, 2024 jijini Mwanza kikiwa na lengo la kujadili utendaji kazi katika Sekta ya umeme.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Bodi ya  TANESCO kuagizwa kumuondoa Meneja Mkuu wa ETDCO kutokana na utendaji mbovu wa kazi ndani ya Taasisi na kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya umeme ukiwemo wa usafirishaji umeme kutoka Tabora hadi Urambo na Tabora hadi Mpanda.

Dkt. Biteko ameagiza Watumishi wote wanaojihusisha na wizi ndani ya Shirika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria ikiwemo kuwaweka pembeni katika Utumishi maana wao ni sababu ya watanzania kutokupata umeme wa uhakika

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amewataka watendaji wa TANESCO kujirekebisha wao wenyewe na wasisubiri kurekebishwa kwani yapo maeneo ambayo wanaweza kusimamia bila kusubiri viongozi ikiwemo kuwafanya watumishi walio chini kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi.

Pia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio ameweka msisitizo kwa Watendaji wa TANESCO kuwa lazima wabadilishe taswira ya Shirika hilo kwa wananchi kwa kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora.

Baadhi ya Watendaji wa TANESCO kwenye kikao hicho wamekiri kuwa taswira ya Shirika hilo kwa wananchi bado inahitaji kuboreshwa ili kuweza kuaminika zaidi kwa wananchi ikiwemo taarifa mbalimbali zinazotolewa na Shirika hilo.
 

HABARI ZAIDI

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

Kituo cha kupoza umeme kujengwa Tunduma

Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Bukombe, akizungumza na abiria

"Fungeni mikanda muda wapo safarini" - SSP