
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla.
Mabula ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara mkoani Simiyu na kutembelea eneo linalojengwa mradi wa maji uliyopo Halmashauri ya Busega Mkoani Simiyuya.
Eneo hilo lilichukuliwa na halmashauri hiyo baada ya mmiliki wake wa awali kujimilikisha kinyume cha sheria na kwa kutumia njia za kidanganyifu kujipatia ardhi.
Mwanzoni mwa mwaka huu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa mkoani Mwanza alifuta hati za viwanja 15 vilivyokuwa vinamilikiwa na Hermant Patel na kurejesha umiliki wake kwa serikali.
Miongoni mwa maeneo aliyonyang’ang’anya Hermant Patel ni eneo hilo linalojengwa mradi wa maji baada ya serikali kuamua kulirudisha Serikalini ambapo Halmashauri ya Busega iliamua kulipangia matumizi hayo.
Aidha, Mhe. Angeline Mabulla amezitaka halmashauri zote nchini kufuata mfano wa Halmashauri ya Busega kwa kuyapima maeneo ambayo yamechukuliwa kutoka kwa wamiliki ambao wameghushi nyaraka na kuzipangia matumizi.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla anaendelea na ziara yake ya mikoa ya kanda ya ziwa ambapo anataria kufanya ziara Mkoani Geita na Shinyanga mara baada ya kumaliza ziara zake mkoani Simiyu.