
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, William Mwampaghale
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera William Mwampaghale, amesema kuwa ajali hiyo imeyahusisha gari la mizigo lililokuwa likitokea nchini Rwanda kwenda Dar es Salaam, likiendeshwa na Vicent Gakuba (52) raia wa Rwanda, na Toyota Succeed lililokuwa likitokea eneo la Nyamalagala wilayani Biharamulo kuelekea Benaco wilayani Ngara likiendeshwa na Nyawenda Bihela (35) ambaye alifariki wakati wa ajali hiyo.
"Uchunguzi wa awali umeonesha ajali hiyo imetokana na uzembe wa dereva wa lori kutokana na kuhama kutoka upande wa kushoto wa barabara na kuendesha gari upande wa kulia, kitendo kilichosababisha magari hayo kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo hivyo, miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, katika kituo cha afya Nyakanazi Biharamulo" amesema Kamanda William.
Kamanda huyo amesema kuwa mbali na dereva pia watu wote waliokuwa katika gari aina ya Toyota Succeed walipoteza maisha, na kutaja majina yao kuwa ni Jesca Leonard (45), Magreth Sekanabo (14), Adidas Sekanabo (12), Zabron Sekanabo (6), Vedastina Sekanabo (8), Michael Charles (28) na Majaliwa Kanundo (32).