Mhe. Nape Nnauye, Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari
Waziri Nape ametoa rai hiyo wakati akifungua mkutano uliokusanya kamati ya maudhui ya ndani kutoka TCRA, vyuo mbalimbali vinavyotoa elimu ya habari, waandishi, wazalishaji wa filamu sambamba na wimiliki wa mitandao wanazalisha na kusambaza Habari.
Nape amesema tuna Lugha ya pekee ya kiswahili ambayo kama wadau wataamua kuitumia inaweza kupata maudhui ambayo yatauzwa nchi katika nchi zote za SADC huku Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA akisema lengo ni kufikia uchumi wa kidigitali ili kuendelea kukuza maudhui ya ndani.

