Alhamisi , 18th Jul , 2019

Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi, Mh Nape Nnauye, amefunguka kuwa yupo jimboni kwake anaendelea na shughuli za maendeleo.

Mbunge wa Mtama Nape Nnauye (Kulia).

Nape ambaye ni Katibu mstaafu wa Itikadi na Uenezi wa CCM taifa, ametoa maelezo hayo leo ikiwa ni siku moja tangu ziibuke sauti mitandaoni zinazodhaniwa kuwa ni yake na katibu mkuu mstaafu wa CCM Abdulrahman Kinana.

''Niko jimboni nakagua utekelezaji wa ahadi na kuboresha maisha ya wana Mtama!'', amendika Nape kupitia Twitter.

Mara kadhaa EATV&EA Radio Digital, imemtafuta Nape kwenye simu yake ya mkononi ili kupata ufafanuzi juu ya sauti hizo zinazosambaa mitandaoni lakini hapokei na mara nyingine anakuwa hapatikani.