Jumatano , 5th Aug , 2015

Mgombea wa Urais kupitia chama cha Mapinduzi Mh. Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Watanzania wana mategemeo makubwa ambayo endapo watampa ridhaa ya kuendesha nchi atawatumikia kufikia Malengo yao.

Mgombea mteule wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, akizungumza na wananchi kwenye viwanja vya Ofisi Ndgo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba.

Akihutubia Umati wa Wanachama na Wanachi waliojitokeza kumpokea baada ya kwenda kuchukua fomu ya kuwania nafasi jana, Katika ofisi ndogo za CCM, zilizopo lumumba jijini Dar es Salaam Magufuli amesema shida zote za Watanzania anazifahamu na atazishgulikia.

Magufuli amesema kuwa kila akiangalia haoni Mtu wa kushindana nae na kumshinda katika uchaguzi huo utakaovishirkisha vyama vingi huku yama vikuu vyenye nguvu vinne vikiungana kwa ajili ya kukitoa chama tawala madarakani.

Amesema Serikali ya Awamu ya nne imefanya mambo mengi yakiwemo ya ujezni wa barabara ambazo pia wapinzani wanazitumia kupita hivyo akishinda ataziendeleza.

Akizungumza baada ya kumpokea Mwenyekiti wa chama hicho Dkt. Jakaya Kikwete amewahakikishia wanachama wa chama hicho kuwa wataibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu kutokana na sifa nzuri ya Chama hicho.