Jumatano , 1st Jun , 2016

Wizara ya Mambo ya Ndani imewahakikishia Watanzania kuwa nchi iko salama licha ya changamoto mbalimbali zinazoendelea ikiwemo matukio ya mauaji pamoja na wimbi la Wahamiaji haramu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhandisi Hamad Yusuph Masauni,

Hayo yamezungumzwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamad Yusuph Masauni, mjini Dodoma, mara baada ya kufanya mkutano na wakuu wa vyombo vilivyopo ndani ya wizara hiyo.

Mkutano huo ulihusisha Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza ,Zimamoto na Uhamiaji ambapo wamejadili tatizo la uingiaji la wahamiaji haramu pamoja na mambo mengine ya Usalama wa Nchi.

Mhe. Masauni amesema kuwa jeshi la polisi limejipanga kudhibiti usalama wa nchi kwa hali yoyote na kwa wale wanaotaka kufanya uhalifu wajue hawataweza kupona huku akitoa maagizo kwa askari wanaokwamisha juhudi za wizara hiyo kuchukuliwa hatua mara moja.