Jumatatu , 29th Nov , 2021

Wafugaji wa jamii ya Kimaasai waliopo Chalinze, Kata ya Ubena mkoani Pwani, wanalazimika kuwanywesha uji Ndama (Mtoto wa Ng'ombe) wao kufuatia maeneo wanayotumia kulishia mifugo kukumbwa na hali ya ukame na kusababisha ng’ombe kushindwa kutoa maziwa.

Wafugaji wakiwanywesha Ndama uji

Wafugaji hao wamesema kwamba hali iliyopo sasa ni ngumu kwao, kwani ukame umewaathiri na kupelekea baadhi ya mifugo kufa, huku wengi wakijitahidi kuwanusuru kwa kuwalisha pumba.