Jumapili , 6th Nov , 2022

Ndege ya abiria ya kampuni ya Precision Air imeanguka ndani ya Ziwa Victoria Bukoba mkoani Kagera asubuhi hii ya leo Novemba 6, 2022. 

Eneo ambalo ndege ya Precision Air imeanguka ziwa Victoria Bukoba na shughuli za uokoaji zikiendelea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amethibitisha ambapo amesema imeanguka ndani ya Ziwa Victoria baada ya kushindwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba.

Ameongeza kuwa kwasasa wanaendelea na uokoaji, taarifa kamili atatoa baadaye. Zoezi la uokoaji linafanywa na Zimamoto, JWTZ wakishirikiana na wavuvi.

Endelea kufuatilia taarifa zaidi kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii.