Ndugai atoa tamko kwa Mawaziri na wabunge

Jumatano , 21st Apr , 2021

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai ameagiza mawaziri, manaibu mawaziri na wabunge, kurudi bungeni mara moja ili kuhudhuria hotuba ya Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hapo kesho.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai

Spika ametoa maagizo hayo mapema leo Aprili 21, 2021, bungeni kwenye mkutano wa tatu kikao cha kumi na nne, ambapo amesema watachukua mahudhurio kwa kuwa kila mtu anatakiwa kuwa ndani ya Bunge wakati Rais anazungumza na taifa.

Katika kipindi cha maswali na majibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba amesema serikali inaibadilisha sekta ya kilimo kutoka kuwa ya kubahatisha kwenda kwenye sekta ya uhakika kwa kuwa sekta hiyo kwa sasa imekuwa ikiongoza kuwa na mikopo chechefu.
 

Tazama video hapo chini