Jumatatu , 13th Mei , 2019

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia amewataka Watanzania kuacha kulalamika juu ya Serikali kutumia gharama kubwa kwenye uchaguzi wa marudio, akisema suala hilo ni kwa mujibu wa Katiba.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia.

Dkt. Kihamia ametoa kauli hiyo wakati alipokutana na wafanyakazi wa NEC kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya tume.

Watu wajifunze kuwepo kwa nafasi wazi ni nini maana watu wanalalamika kwamba Serikali inatumia fedha nyingi kufanya chaguzi ndogo za mara kwa mara lakini wanasahau kwamba suala hilo lipo kwenye katiba na ni utarabu.” amesema Dkt. Kihamia.

Aidha amesema katika kipindi alichokaa kwenye tume, amegundua kuwa sasa utendaji kazi wa mazoea umepungua na watumishi wengi wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa wakati.

Tuligundua kuwa changamoto nyingi zilitokana na tabia binafsi za baadhi ya watumishi, na baadhi yao kufanya kazi kwa kuigiza yaani kwa mazoea kwa kisingizio cha mchakato”, ameongeza Dkt. Kihamia.