Jumatano , 16th Dec , 2015

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Utumishi na Utawala bora George Simbachawene amewataka watendaji wa wizara hiyo kufanya kazi kwa kufuata maadili na kuacha kufanya kwa mazoea ili kuharakisha maendeleo.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene.

Akizungumza na Watendaji Mjini Dodoma Waziri Simbachawene amesema kuwa sasa ni wakati muafaka kwa watendaji kuwajibika ipasavyo ikiwemo kutoka maofisini na kutembelea sehemu mbalimbali zenye kero kwa wananchi ili kuzishguhulikia haraka.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa wizara hiyo Mh. Suleiman Jaffo amesema kuwa endapo kila mmoja akiwajibika ipasavyo malengo ya serikali ya awamu ya tano yataleta ufanisi wa haraka.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw, Jumanne Sagini amesema licha ya changamoto wanazokabiliana nazo lakini maelekezo yaliyoanza kutolewa yameanza kuzaa matunda katika baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa na malalamiko.