Jumanne , 6th Sep , 2016

Nigeria imetangaza mtu wa tatu wa maradhi ya kupooza katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wakati Shirika la Afya Duniani (WHO) likionya juu kuwepo na hatari ya kuongezeka kwa wagonjwa wa maradhi hayo.

Ramani ya Nigeria

Kwa mujibu wa msemaji wa shirika la kimataifa la Rotary, Stephanie Mucznick amesema wagonjwa wote watatu wanaougua maradhi hayo wanatoka katika maeneo ya Kaskazini Mashariki ambayo yamekuwa yakikumbwa na maradhi hayo kwa miaka kadhaa sasa.

Afisa huyo amesema kisa cha hivi karibuni kinamhusu mtoto wa umri wa miaka miwili ambaye aligundulika kuugua maradhi hayo Agosti 6, mwaka huu.

Maradhi ya kupooza huwakumba zaidi watoto wadogo na hayana tiba inagawa yanaweza kuzuiwa kwa njia chanjo pekee

Makao Makuu ya WHO