Jumapili , 5th Jul , 2020

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana wa ACT Wazalendo Abdul Nondo amesema kuwa hakuona haja ya yeye kumshirikisha Zitto Kabwe kama anataka kutia nia ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Kigoma Mjini  kwa kuwa chama hicho kinazingatia demokrasia na kwamba hakina Papa bali wanachama wote ni sawa.

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo, Abdul Nondo.

Abdul Nondo ametoa kauli hiyo leo Julai 5, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kusema kuwa endapo vikao vya chama chake vitampa ridhaa ya kupeperusha bendera ya kugombea Ubunge, basi atahakikisha anatekeleza na kuyaendeleza yale yote aliyoyaanzisha Mbunge mstaafu wa jimbo hilo Zitto Kabwe.

"Inawezekana mimi nikachaguliwa na Zitto akaachwa kwa sababu chama chetu kinaongozwa kwa mfumo wa demokrasia ya wazi, kwahiyo wajumbe wanaweza wakaamua kwa sababu chama chetu hakina Papa, kinasema wote ni sawa haijalishi wewe ni nani, Wajumbe wanaweza wakaamua kunichagua mimi, au wakaamua kumchagua Zitto halafu mimi wakaniambia nisubiri" amesema Nondo.

Leo Julai 5, 2020, Abdul Nondo ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Kigoma Mjini, ambalo kabla ya Bunge kuvunjwa, lilikuwa likiongozwa na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe.

Tazama Video hapa chini.