Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

AUDIO : Niyonzima afunguka kifo cha Ndikumana

Jumatano , 15th Nov , 2017

Mchezaji wa Klabu ya Simba raia wa Rwanda Haruna Niyonzima amefunguka na kusema kuwa kinachodaiwa kupelekea kifo cha Mchezaji mwenzake Hamadi Ndikumama ni maumivu ya kichwa.

Akizungumza na EATV Website, Niyonzima amesema kuwa taarifa za awali azilipotokea kutoka Rwanda, zimesema kwamba Ndikumana alianza kupata maumivu ya kichwa  jioni mara baada ya kumaliza mazoezi kwenye timu yake.

Haruna amesema kwamba "Ndikumana hakuwa mgonjwa bali kwa taarifa nilizopokea ni kwamba alianza kuumwa na kichwa baada ya kumaliza mazoezi jana jioni. Alidhani ni maumivu ya kawaida kwamba na baadae yatakwisha lakini baadae yalimzidia na kuamua kwenda hosipitali na ndipo alipofariki usiku wa kuamkia leo.

Ameongeza "Ninachofahamu mimi Ndikumana alikuwa na maradhi ya moyo lakini nikipata tarifa zaidi kutoka kwa watu walipo nyumbani nitajua zaidi nini chanzo"

Kabla ya kufikwa na umauti Katauti alikuwa kocha msaidizi wa kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda, enzi za uhai wake aliwahi kuichezea klabu ya Stand United ya Shinyanga akitokea timu ya Cyprus.

Ndikumana amewahi kuwa Mume wa muigizaji Irene Uwoya ambapo walifunga ndoa mwaka 2009 na kujaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume (Krish) kabla ya kutengana baadaye.

Msikilize hapa chini Niyonzima akielezea.

HABARI ZAIDI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama

Wazazi simamieni maadili kwa watoto 

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa