Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda
Paul Makonda amedai katika mambo ambayo yalielezwa na wasanii hao ni asilimia 25 tu ambayo yalikuwa na msingi lakini lakini asilimia nyingine zikiwa hoja ambazo hazina mashiko.
"Nimesikiliza kama mwanazuoni nikaona asilimia 25 ni mawazo ya kujenga na asilimia 75 si kitu na wengine mmepata fursa ya kuongea hapa mnaleta stori za vijiweni hapa mbele yangu."
"Nilikuwa namsikiliza Nikki hapa nikagundua hanifahamu kwa hiyo ukisema tunakuja dakika za mwisho kupaisha wewe ndiye unapaisha kwa sababu hamuelezi mambo ya msingi."
Awali Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es salaam alisema Mkoa wa Dar es salaam umetenga zaidi ya shilingi bil 2 kwa ajili ya kuwasaidia wasanii ili waweze kuinuka kisanaa.





