Mwaka 1985 volcano ililipuka huko Columbia na kuteketeza kijiji cha Armero. Miongoni mwa wahanga wa tukio hilo ni binti Omayra Sanchez aliyekuwa na miaka 13. Mpiga picha Frank Fournier alimpiga picha hii akiwa amekwama kwenye matope, majivu na maji. Waokoaji walijaribu kumtoa lakini waligundua kuwa miguu yake imekwama kwenye paa la nyumba yao iliyokuwa imebomolewa na volcano, na chini yake kulikuwa na maiti ya shangazi yake ambaye alifariki. hivyo kumtoa bila kujeruhi isingewezekana, Walimuwekea mpira ili asizame huku wakendelea kutafuta njia mbadala ya kumtoa, walikuwa wakihofia iwapo watamtoa lazima watamvunja miguu na huduma za afya hazikuwa zenye ubora. Aliwaambia waokoaji wamuache wapumzike na kumuomba mpiga picha ampe chakula kitamu na soda.
Omayra alifariki baada ya kukaa kwa siku tatu kwenye tope hilo.