
Spika Mstaafu wa Pius Msekwa
Spika huyo mstaafu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na www.eatv.tv pale alipoulizwa juu ya miaka mitatu ya Rais wa Magufuli na kutenguliwa kwa mawaziri walioshindwa kuendana na kasi yake.
Msekwa amesema "naomba wamsikilize Rais mwenyewe alisema hata akibaki na waziri mmoja, hii haki yake ya kikatiba, hata wewe bosi wako, akikubadilisha utahoji kwanini? ni majukumu yake ya kikatiba msilinganishe na viongozi wengine waliopita."
Jana akiwaapisha Mawaziri wa wizara mbalimbali nchini Rais Magufuli alitaja sababu ya kuwatumbua waliokuwa mawaziri wa kilimo, pamoja na viwanda na biashara
"Nilimwambia Waziri Mkuu awakumbushe mawaziri wake, kwa sababu matatizo mengi yaliyokuwa yakihusu kilimo na viwanda yalikua yanamalizwa na Waziri Mkuu, nilijiuliza pia kahawa ni kilimo pia vipi Waziri hakuliona pia." Alisema Rais Magufuli.
"Nilijiuliza kwanini hawa tuliowapa ,majukumu hawafanyi hivi, ni ukweli pia bei ya soko la korosho limeshuka kidogo unapoona kuna tatizo unamtuma Waziri Mkuu anatatua," aliongeza Rais Magufuli.