Alhamisi , 2nd Jun , 2022

Jeshi la Polisi Arusha limesema kwamba kwa kushirikiana na vyombo vingine limeanza kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha kifo cha fundi gereji Kibabu Msese (26), ambaye hali yake ilibadilika ghafla akiwa kituo cha polisi Karatu na kukimbizwa hospitali.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Justine Masejo

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo, ambapo amesema Msese alikuwa ni miongoni mwa watu wanne waliokamatwa kwa tuhuma za kupora milioni 14.5, simu kadhaa pamoja mashine za uwakala wa benki mali za mfanyabiashara wa M-PESA Manyara, tukio wanalodaiwa kulifanya Mei 11 mwaka huu.

Kamanda Masejo ameongeza kuwa, wakati wa mahojiano watuhumiwa hao walionesha baadhi ya mali zillizoibiwa pamoja na silaha waliyokuwa wanaitumia katika tukio hilo ambapo pia walikiri kushiriki matukio kadhaa nje na ndani ya mkoa na walifikishwa mahakamani Mei 27 mwaka huu na wengine wanaendelea kutafutwa.