
Serikali inasema usambazaji wa mafuta utaanza kurejea tena katika hali yake ya kawaida kutoka kituo cha Varreux, katika eneo la Cité Soleil.
Magenge hayo yaliteka kituo hicho cha bandari mwezi Septemba, na kuzuia utoaji wa mafuta kutoka nje na kukwamisha juhudi za kusambaza chakula na dawa.
Kituo hicho kinasambaza bidhaa nyingi za mafuta nchini Haiti.
Sehemu hiyo Imedhibitiwa na kuzuiwa na muungano wa magenge yenye nguvu, unaojulikana kama G9, kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Kizuizi hicho kimelazimisha wafanyabiashara wengi kufunga na kutatiza usambazaji wa mafuta ya petroli na maji ya kunywa ya chupa, huku mlipuko wa kipindupindu ukizidi kuwa mbaya kwa wiki nzima.