Jumatatu , 30th Dec , 2019

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu 2, akiwemo Msaidizi wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, aliyejulikana kwa jina la Abdulkarimu Muro na Saidi Haidani, ambaye pia ni Dereva wa Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika.

Abdulkarimu Muro (Msaidizi Katibu Mkuu CHADEMA) na Saidi Haidani Dereva wa Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika.

Polisi wameeleza waliwakamata watu hao jana Disemba 29, 2019, Mtaa wa Mahina - Nyamagana kufuatia wananchi kuwa na mashaka nao.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo imesema, watu hao waligoma kujitambulisha awali na kupelekea Jeshi la Polisi kudhani watu hao walikuwa na nia ovu.

Aidha Jeshi hilo limekanusha juu ya madai ya kutekwa kwa watu hao wawili, kama ilivyodaiwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii, usiku wakuamkia leo Disemba 30.