
Jeshi la polisi
Akizungumza na wandishi wa habari mapema leo Kamanda wa Jeshi hilo Juma Bwire amesema wamejipanga vyema kufanya doria za nguvu na misako kila mtaa kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama katika Mkesha wa mwaka mpya na kutoa rai kwa wananchi.
Kwa upande wao wananchi wameeleza namna walivyojipanga kuupokea mwaka mpya pamoja na changamoto zilizowakabili katika mwaka 2018.
Katika hatua nyingine Kamanda Bwire amesema katika kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba 2018 jeshi hilo limefanikiwa kupunguza matukio ya uhalifu kwa asilimia 5.7
Katika mkesha huo wa mwaka mpya bwire amesema fataki zitapigwa katika eneo moja pekee na kwa yeyote atakayefanya hivyo bila kibali maalumu hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Mbali na Kamanda Bwire Jijini Dar es salaam Kamanda Mambosasa pia amepiga marufuku watakaojipanga kurusha mafataki nyakati za usiku.