Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilim
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilim amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika oparesheni maalumu iliyofanyika kuanzia septemba 12 mwaka huu katika maeneo ya Kihonda, chamwino mkundi, Tungi, Nanenane, Mbuyuni Msamvu, Mafisa na manyuki ambapo wananchi wa maeneo hayo walikuwa wakilalamikia vijana hao kuwapora mali zao kwa kutumia pikipiki na siraha za jadi.
Aidha kamanda Musilimu amesema kuwa katika zoezi la usalimishaji wa siraha za moto zinazomilikiwa na wananchi kinyume cha sheria jumla ya siraha 6 zimeshasalimishwa na kuwanataka wananchi kutumia muda uliotolewa na serikali wa kuanzia septemba 1 hadi octoba 31 mwaka huu kuasalimisha siraha hizo kwa hiyari ambapo hawatachukuliwa hatua za kisheria.

