
Prof. Kitila Mkumbo
Prof. Mkumbo ambaye pia ni kada na mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo kinachoongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema Rais amempa heshima kubwa kwa nafasi hiyo, na yeye kama mtumishi wa umma hawezi kuikataa kwa kuwa ni kazi aliyotumwa na mkuu wa nchi.
"Ukishapewa kazi na mkuu wa nchi, unaipokea na unaifanya kwa bidii kama yalivyo matarajio, kwahiyo nimepokea uteuzi, nimekubali, mkuu wa nchi akikupa kazi utaikataa vipi, mkuu wa nchi akikupa kazi unaifanya, kumbuka mimi ni mtumishi wa umma" Amesema Prof Kitila wakati akizungumza na EATV kwa njia ya simu.
Msikilize hapa