.jpg?itok=t7MG7qWl×tamp=1473579164)
Hayo yamesemwa na mtafiti na mchambuzi wa masuala ya uchumi nchini Prof. Haji Semboja wakati wa uwasilishwaji wa fahirisi za bei kwa mwezi wa kwanza 2016 unaofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dar es Salaam.
Prof Semboja amesema agizo la kupanga bei lisiwe la muda mrefu na kuwa soko la kimataifa linategemeana hivyo mazingira ya biashara yanapaswa kutoa fursa na sio kufunga mipaka kwani kwa kufanya hivyo kutaathiri soko la biashara.
Naye Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii Siasa ya Watu kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephrahim Gwesigabo amesema mfumuko wa bei kwa mwezi Aprili 2016 umepungua ikilinganishwa na mwaka jana mwezi Aprili kutokana na kushuka kwa bidhaa za nishati ikiwemo Gesi na Mafuta.