Jumatano , 27th Jan , 2016

Jeshi la polisi nchini Senegal limewakamata raia 900 katika oparesheni ya kukabiliana na ugaidi nchini humo.

Kamata kamata hiyo imefanyika katika mji mkuu wa Dakar karibu na mtaa wa Thies. Jeshi la ulinzi limetoa angalizo tangu shambulio lilipotokea mapema mwezi huu katika hoteli iliyoko mji mkuu wa Burkina Faso, ambapo watu thelathini waliuawa.

Aidha wiki iliyopita waziri wa mambo ya ndani Abdoulaye Daouda Diallo alizitaka hoteli zote nchini humo kuongeza ulinzi.

Chanzo BBC