Jumanne , 3rd Nov , 2020

Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu Jijini Dar es salaam, imemhukumu raia wa Msumbiji Rashid Athuman Rashim, mwaka mmoja jela au kulipa faini ya shilingi milioni nne katika makosa mawili ikiwemo kuingia nchini bila kibali.

Pichani mtu akiwa amefungwa pingu (Picha kutoka mtandaoni)

Hukumu hiyo imetolewa hii leo na Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando na kusomewa mashtaka na wakili wa serikali Sitta Shija.

"Faini milioni mbili kwa kila kosa au kwenda jela miezi sita kwa kila kosa" amesema Mmbando

Katika kesi hiyo mshtakiwa anadaiwa kuingia na kukutwa akiishi nchini bila kibali ambapo alikiri kutenda kosa hilo.

Aidha mshtakiwa ameshindwa kulipa faini hiyo na amerejeshwa rumande.